October 21, 2016

AKILIMALI (KUSHOTO)...

Pamoja na kuibuka na kushikilia msimamo kuwa anapinga suala la klabu ya Yanga kukodishwa kwa miaka 10 kwa kampuni ya Yanga Yetu Ltd, taarifa zinaeleza Ibrahim Akilimali si mwanachama wa Yanga.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zinaeleza Akilimali ambaye ni katibu wa baraza la wazee wa Yanga, si mwanachama kwa kuwa hajalipa ada kwa zaidi ya miezi miaka sasa.

“Ni kweli, mara ya mwisho alilipiwa na Mwenyekiti (Manji), baada ya hapo hajawahi kulipa ada hata mara moja. Kwa mujibu wa katiba ya Yanga, yeye si mwanachama wa Yanga,” alisema mmoja wa wapasha habari.

Juhudi za kumsaka Akilimali zilifanyika, alipopokea simu akasema: “Nani kakuambia, mbona mnanifuatafuata hivyo, tafadhari mniache, nisipokuwa mwanachama, halafu?” Baada ya hapo alikata simu na ikawa haipatikani.

Akilimali amekuwa mstari wa mbele kuweka msimamo wake kwamba Yanga isikodishwe lakini kumekuwa na barua zinazosamabazwa mitandaoni zikionyesha Akilimali akiweka msisitizo katika suala la Yanga kuwa kampuni.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV