Kikosi cha Kilimanjaro FC cha Sweden kimepanda hadi daraja la sita.
Kilimanjaro FC inaongozwa na Watanzania wanaoishi nchini humo na kati ya kiungo wao tegemeo ni Shekhan Rashid na mshambuliaji mahiri, Athumani Iddi Machuppa.
Hawa wote waliwahi kuichezea Simba na Taifa Stars, sasa wanaendelea maisha yao nchini Sweden lakini wamepata muda wa kuichezea timu hiyo inayomilikiwa na Watanzania.
Pichani, Shekhan akiwa na mkewe na wanaye wakifuarahia baada ya kazi hiyo nzuri.
Saafi, Wanaitangaza nchi yetu vema
ReplyDelete