October 3, 2016



Hii hatari aisee, Licha ya kwamba mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo hakufunga bao walipoumana na Yanga wiki iliyopita, lakini amesema si timu ya kutisha sana, anaiona ya kawaida na zaidi walikuwa na bahati wamenusurika kuchezea kichapo licha ya wao kuwa pungufu.

Mavugo amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar na kuisha kwa sare ya 1-1 ambapo alikiri kuwa Yanga ni timu kubwa lakini haitishi kama inavyoelezwa zaidi ya kutegemea uwezo wa mchezaji mmojammoja.

“Sikatai Yanga ni timu kubwa, nilikuwa nikisikia Yanga ni wazuri sana, leo (juzi) nimekutana nao, si wabaya lakini zaidi ni uwezo wa mchezaji mmoja mmoja kwa jinsi nilivyowaona leo (juzi) na kama tungekuwa tumetimia, Mkude (Jonas) asingepewa nyekundu, tungewafunga bila tatizo.

“Muda mwingi tuliwazidi, ukiangalia kipindi cha pili chote tulicheza pungufu lakini tulicheza vizuri zaidi yao na tukafunga bao tukiwa wachache. Kuhusu kutofunga leo, huwa inatokea na mechi yenyewe, muda mwingine unaweza kupanga hivi na ikawa tofauti,” alisema Mavugo aliyefunga mabao matatu mpaka sasa.

Katika mchezo huo, Mavugo aliyewahi kuichezea Vital’O ya Burundi, alipata nafasi ya kupiga mashuti matatu katika lango la Yanga, yote hayakuwa na madhara na yalipita nje ya lango.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic