October 3, 2016Bao la kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya, limezuia Sh milioni 60 ambazo waliahidiwa kupewa wachezaji wa Yanga kama wangewafunga watani wao wa jadi.

Kichuya alilifunga bao hilo la kusawazisha dakika ya 87 ya mchezo huo baada ya kupiga kona ya moja kwa moja huku ikimshinda kipa, Ally Mustapha 'Barthez'.

Bao hilo la lala salama lilisababisha mchezo huo umalizike kwa sare ya bao 1-1.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata wachezaji hao waliahidiwa fedha hizo kama wangeifunga Simba na siyo sare ya aina yoyote.

“Wachezaji wetu tuliahidi kuwapa shilingi milioni 60 kama posho kama wangewafunga Simba. Lakini wameshindwa kutimiza hilo, hivyo uongozi hautatoa fedha zozote kwani wameshindwa kutimiza kile tulichokuwa tunakitaka.


"Kama unavyojua, mechi hii kama tungewafunga Simba, tungekuwa tumebakiza pointi chache ili kuwaondoa kileleni, hivyo tumeshindwa kuzipunguza pointi hizo, hivyo kama viongozi tunasikitika katika hilo," alisema mtoa taarifa huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV