October 13, 2016


Baada ya kucheza mechi nane, Shiza Kichuya hadi sasa ndiye mshambuliaji hatari zaidi katika Ligi Kuu Bara.

Kichuya ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, ameishapachika mabao sita.

Mabao hayo yanamfanya aongoze msimamo wa wafungaji na kuwafunika kabisa washambuliaji wa kigeni.

Kichuya amewafunika wageni katika kikosi chake ukianza na Frederick Blagnon ambaye hana bao na Laudit Mavugo ambaye amefunga mabao matatu.

Kama hiyo haitoshi, Kichuya amewafunika washambuliaji wa kigeni pia katika timu nyingine ikiwemo Yanga ambayo ina Amissi Tambwe mfungaji bora wa msimu uliopita na Donald Ngoma.

Kichuya ambaye asili yake kiungo, ameisaidia Simba kushinda mechi sita katika ya nane ilizocheza za ligi hiyo.

Hata hivyo, inaonekana ushindani bado ni mbichi kabisa kwa kuwa washambuliaji hao wa kigeni hasa wale wa Yanga, wanaweza kuubadili “mchezo” wakati wowote.


1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV