October 8, 2016


HANS POPPE

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya apewe ofa ya gari na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Zacharia Hans Poppe, mchezaji huyo ameibuka kuizungumzia ofa hiyo.

Hans Poppe amefikia hatua hiyo baada ya kuridhishwa na uwezo wa Kichuya tangu kuanza kwa msimu huu Ligi Kuu Bara, akikumbukwa zaidi kwa mabao yake mawili, moja dhidi ya Azam FC na lingine la wikiendi iliyopita dhidi ya Yanga.

Kichuya alifunga bao pekee la Simba katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam pia Jumamosi iliyopita aliifungia timu yake bao la kusawazisha dhidi ya Yanga na kupata sare ya bao 1-1.
KICHUYA AKIWA AMEBEBWA
Kichuya, mwenye mabao matano katika ligi, alisema kama atapewa gari na Hans Poppe atashukuru lakini hawezi kuifurahia zawadi hiyo endapo Simba itafanya vibaya.

Alisema lengo lake tangu anajiunga na Simba ni kuisaidia kufanya vizuri ili ibebe ubingwa wa ligi kuu na michuano mingine itakayoshiriki ikiwemo Kombe la FA.

“Siwezi kupinga kupewa ofa hiyo ya gari lakini binafsi siwezi kucheza kwa ajili ya gari, ishu ya kuipigania Simba nilikuwa nayo tangu natua hapa, dhumuni langu kubwa ni kupigana kwa ajili ya Simba.


 “Furaha yangu ya kwanza ni kuifikisha pazuri Simba msimu huu kisha kama kutakuwa na mengine kama hizo zawadi za magari zitafuata nyuma ya hiki ninachofanya sasa,” alisema Kichuya aliyetua Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar.Ahadi hiyo ikitimia, Kichuya atakuwa mchezaji wa pili kupewa gari msimu huu baada ya awali, beki wa kushoto wa timu hiyo, Mohammed Hussein Zimbwe Jr ‘Tshabalala’ kupewa gari aina ya Toyota Raum wiki nne zilizopita.

1 COMMENTS:

  1. Matamushi ya Shiza Kichuya ni matamushi ya mtu anayejua kweli kilicho mpeleka Simba. Ni wachache sana manyota wa Tanzania wenye hulka hii! Zawadi ni sehemu ya motisha. Lakini, haina maana kwa mpokeaji kama lengo la mtoa motisha halitafikiwa mwishoni mwa yote. HONGERA KICHUYA, VUTA SOKSI NYOTA IKUPELEKE UTAKAKO KUFIKIA KISOKA!

    VIVA SIMBA SC

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic