Kasi ya ufungaji wa kikosi cha Simba unaonekana kuwa wa kuotea mbali baada ya kufikisha mabao 15 katika mechi nane.
Idadi hiyo inaifanya Simba kuwa na karibu wa wastani wa mabao mawili kwa kila mechi na kuifanya kuwa timu hiyo kuwa na mwenendo mzuri zaidi kwa mabao ya kufunga.
Simba imefikisha mabao hayo baada ya kuitwanga Mbeya City kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Yanga inaifuatia Simba kwa kuwa na mabao 12 ikiwa imecheza mechi saba, hivyo kuwa na wastani usiopishana sana na Simba.
Yanga imejiongezea idadi ya mabao ya kufunga baada ya kuichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 3-1.
Lakini bao hilo moja, linaifanya Yanga kufikia mabao matatu ya kufungwa kama ilivyo kwa watani wake Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment