October 28, 2016


KICHUYA

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe, amesema mbio za ufungaji bora kwenye Ligi Kuu Bara ni ngumu kutokana na ushindani uliopo lakini ameahidi atapambana kuiwezesha Yanga kufanya kweli na ikibidi yeye kutetea tuzo yake ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mrundi huyo, ambaye kwenye mechi ya juzi ya ligi kuu dhudi ya JKT Ruvu alifunga mabao mawili akitokea benchi, sasa amefikisha mabao sita ikiwa ni moja nyuma ya Shiza Kichuya wa Simba anayeongoza akiwa na mabao saba.  

Kwa kasi hiyo na kwa tambo hizo ni wazi Tambwe amempa angalizo Kichuya kuongeza bidii la sivyo atampita na yeye kushika usukani wa kuongoza kwa mabao katika ligi hiyo.

TAMBWE
Tambwe alisema haikuwa kazi rahisi kufunga mabao mawili juzi kwa kuwa ametoka katika majeraha ya kupasuka kwenye paji la uso katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na kusababisha ashonwe nyuzi sita.

"Kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kufunga mabao mawili, mabao hayo yametokana na juhudi na kujituma kwangu kwa kushirikiana vema na wachezaji wenzangu ambao wamenitengenezea nafasi hizi za kufunga.

"Nimefikisha mabao sita, lakini bado nina kibarua kigumu cha kutetea kiatu changu cha dhahabu kutokana na ushindani mkubwa wa ufungaji mabao, kama unavyoona wachezaji wanajitahidi kufunga mabao, najua Kichuya ana saba ila mimi pia nitaendelea kujituma nifunge zaidi,” alisema Tambwe.


Tambwe aliwahi kutwaa ufungaji bora katika ligi kuu msimu wa 2013/2014 akifunga mabao 19 akiwa Simba, 2015/2016 akipachika 21 akiichezea Yanga huku 2014/2015 akimaliza kwa kushika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji akifumania nyavu mara 14.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic