October 9, 2016


Kocha Mkuu wa Inter Club ya Angola, Zdravko Logarusic, anaonekana hana raha nchini humo.

Siku chache zilizopita, alitupia maneno mtandoni akionyesha “Angola si rahisi”.

Lakini rafiki yake wa karibu, amesema Logarusic, kocha wa zamani wa Simba, ana mpango wa kuondoka Angola.

“Nafikiri kocha ataondoka Angola. Hapafurahii na mambo mengi si sawa,” alisema rafiki yake huyo.


Juhudi za kumpata Loga alizungumzie hilo, zinaendelea na tutawataarifu baada ya kumpata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV