October 6, 2016Mashabiki 42,123 ndiyo waliingia uwanjani kwa kulipa katika mechi ya Jumamosi kati ya Yanga dhidi ya watani wake Simba.

Mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 1-1, Jumla ya Sh milioni 357 zilipatikana kwa mujibu wa kampuni ya Selcom.

Meneja Miradi wa Selcom, Gallus Runyeta amesema hayo ni mapato yaliyopatikana kutumia mfumo wa tiketi za elektroniki.


Aidha, Runyeta alisema mechi zikiwa zinapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, basi watazamaji watakuwa wakitumia mageti ya Uwanja wa Taifa kuingilia uwanjani hapo. Mageti hayo ni B, C na D.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV