October 26, 2016

MAYANJA

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, ameibuka na kusema kuwa, wapinzani wao Yanga wana presha kubwa kwa sasa ya kutaka kuwafikia pointi zao kwenye msimamo wa ligi jambo ambalo ni vigumu kutokana na kiwango cha timu yao kilivyo.

Simba inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 29, huku Yanga ikiwa na pointi 21 pamoja na mchezo mmoja mkononi.

Mayanja amesema kuwa, kwa upande wa timu yao ya Simba hawana presha katika ligi na badala yake wanacheza kuhakikisha wanafanikiwa kushinda katika kila mechi, tofauti na wapinzani wao ambao wana presha kubwa kutokana na pointi walizowapita.

“Yanga ndiyo wenye presha kubwa kwa sasa kutokana na kutaka kufikia pointi nane tulizowapita, hivyo lazima wawe na wakati mgumu wa kuhakikisha wanapigana ili kuweza kutufikia jambo ambalo linawapa shida.
“Kwa upande wetu hatuna presha yoyote ila tunachotakiwa ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwa kushinda katika kila mechi na wasitarajie kutufikia kirahisi.

“Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa na kila timu inahitaji kufanya vizuri na kushinda,” alisema Mayanja.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic