October 5, 2016


Mkurugenzi wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Simba, Haji Manara amepigwa faini ya Sh 200,000.

Kamati ya Bodi ya Ligi ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokaa jana, imempiga Manara faini hiyo baada ya kuingia uwanjani wakati wa mechi ya watani.

Imeelezwa Manara aliingia uwanjani wakati wa mechi ya watani Yanga dhidi ya Simba, eneo ambalo hakuwa akihusika.

Katika picha zinamuonyesha Manara akiwa katika eneo hilo akijaribu kuwatuliza mashabiki wa Simba waliokuwa waking’oa viti.

Kutokana na hali hiyo, kamati imesema imetumia kanuni ya 14(10) kumtwanga Manara adhabu hiyo.


Katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya mabao 1-1 mashabiki wa Simba walicharuka na kung’oa viti baada ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga bao lakini kabla aliunawa mpira, jambo ambalo likaamsha jazba kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV