October 6, 2016Simba imepanga kuondoka mapema jijini Dar es Salaam ili ipate nafasi ya kucheza mechi moja ya kirafiki mkoani Iringa.

Kikosi cha Simba ndiyo kipo kileleni mwa Ligi Kuu Bara na sasa kinaanza rasmi kucheza mechi za mikoani.

Mechi ya kwanza itakuwa dhidi ya Mbeya City Jumatano ijayo mjini Mbeya.

Tayari Kocha Mkuu, Joseph Omog ameeleza kwamba kuna mambo kadhaa ya kubadilisha.

Omog amesema kuna mambo ya kubadilisha kwa kuwa viwanja vya mikoani ni tatizo kubwa na lazima kuwe na mbinu tofauti kiuchezaji.

Katika mechi saba zilizopita, Simba imeshinda tano na kutoka sare mbili hivyo kuifanya iendelee kukaa kileleni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV