Taarifa zimezagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba mwamuzi Martin Saanya kutoka Morogoro amefungiwa miaka miwili.
Saanya ambaye ni askari Magereza aliboronga mchezo wa watani Yanga na Simba kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita.
Taarifa hizo ambazo zinaonekana si rasmi, zinaeleza baada ya kamati ya saa 72 kukaa, imefikia uamuzi huo.
Lakini hakuna kiongozi wa TFF ambaye alitaka kuthibitisha hilo kuhusiana na Saanya.
Pamoja na hivyo, kumekuwa na taarifa kwamba kamati hiyo ilikuwa lazima ikae na kuamua.
Kwamba Saanya na msaidizi wake sasa wamefungiwa huku kukiwa na taarifa za kadi nyekundu ya Jonas Mkude imefutwa.
Lakini kiongozi mmoja wa TFF ambaye amesema si msemaji, amesama haya: “Sipendi unitaje kwa kuwa si msemaji. Lakini ninajua kamati ilikuwa ikae ila sina uhakika.”
Simu za viongozi wote wa TFF zilikuwa hazipatikani, huenda ni kutokana na muda wenyewe wa usiku.
Tunaendelea kufuatilia ili kupata uhakika na kuthibitisha kwamba ni sahihi au la.
0 COMMENTS:
Post a Comment