November 8, 2016Kocha George Lwandamina amesema baada ya kuachia ngazi kuinoa Zesco ya Zambia sasa yuko tayari kwa kazi mpya.

Lwandamina amezungumza moja kwa moja na SALEHJEMBE kutoka Lusaka, Zambia na kusema: "Niko tayari kwa kazi mpya".

"Kweli niko tayari kwa kazi mpya, lakini siwezi kusema ni wapi," alisema.

Alipoulizwa tayari kuna taarifa za uhakika anakuja nchini kwa ajili ya kuinoa Yanga, alisema:

"Kweli? Kama itakuwa hivyo si kitu kibaya. Lakini naweza kukuhakikishia niko tayari kwa kazi mpya."


Kocha huyo ameondoka Zesco kwa kuachia ngazi na ndiyo anatua nchini kesho alfajiri kwa ajili ya kuinoa Yanga na kuchukua nafasi ya Hans van der Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV