November 8, 2016

AME ALI AKIWA NA KOCHA JOSEPH OMOG

Kikosi cha Simba tayari kimetua mjini Mbeya kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons ya Mbeya, kesho.

Lakini wachezaji watatu wameachwa jijini Dar es Salaam kutokana na matatizo mbalimbali.

Ibrahim Ajibu yeye amepata msiba wa mwanaye lakini Abdi Banda anauguliwa na mama yake mzazi huku mshambuliaji Ame Ali ni mgonjwa.

Hivyo Simba itawakosa wachezaji hao watatu katika mechi hiyo ya kesho kufunga mzunguko wa kwanza kwa upande wake.


Simba imekwenda Mbeya ikiwa na majeruhi ya kufungwa bao 1-0 na African Lyon ambayo inaonekana haiko vizuri na haikutegemewa kama ingeweza kuitwanga Simba ambayo ilishacheza mechi 13 bila ya kupoteza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV