November 3, 2016


Yanga imeendelea na mazoezi tena leo ikiwa ni siku moja baada ya kukubali kipigo cha mabo 2-1 kutoka kwa Mbeya City.

Yanga walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na hayakuwa ya muda mrefu.

Kwa sasa Yanga wanajiandaa na mechi dhidi ya Prisons ya Mbeya ambayo itapigwa keshokutwa Jumamosi.


Jana Yanga ilikubali kipigo hicho na kuifanya iwe imepoteza mechi ya pili katika Ligi Kuu Bara. Mechi ya kwanza walifungwa na Stand United kwa bao 1-0.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV