November 11, 2016

BUKUNGU (KULIA), AKIWA NA MGOSI (KATIKATI) NA NDUSHA.

Beki wa pembeni wa Simba, raia wa DR Congo, Besala Bokungu, ameongeza familia baada ya kufanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Bokungu amesema huyo ni mtoto wake wa nne kumpata kati ya hao, wawili wavulana na mmoja wa kike.

Bokungu alisema mtoto wake huyo aliyempa jina la Bestynie alizaliwa usiku wa Novemba 7, mwaka huu huko nyumbani kwao DR Congo.

“Kwanza nianze kwa kumkaribisha mtoto wangu wa kiume duniani baada ya mke wangu kujifungua salama, kikukweli namshukuru Mungu kwa zawadi hii nzuri ya mtoto kutoka kwa mke wangu.

“Mke wangu alijifungua usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita na tayari nimempa jina la Bestynie, kiukweli nimefurahi sana, nimepanga kwenda kumuona hivi karibuni baada ya ligi kuu kusimama,” alisema Bokungu. 
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV