November 19, 2016Taarifa za mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu zimezidi kuzagaa na imeelezwa amepata ajali ya gari akiwa njiani kwenda Dodoma.

Awali kulikuwa na taarifa mbaya kwamba alipoteza maisha lakini baadaye zikathibitika ni za uzushi.

Juhudi za kumpata zilikuwa ngumu, baadaye meneja wake akathibitisha alipata ajali.

“Kweli kapata ajali, gari imeharibika sana. Niliwapigia akapokea mtu simu yake na kuthibitisha, lakini amesema Malimi yuko poa,” alisema.

Baadaye, SALEHJEMBE ilipiga simu ya Busungu, alipokea na kuthibitisha ajali hiyo lakini akasema bado yuko polisi anaandikisha.


“Bado naandikisha hapa, halafu tutazungumza,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV