November 15, 2016Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema pamoja na figisu zote, anaamini hakuna wa kuizuia Simba kuwa bingwa.

Hans Poppe amesema, wanajua kuna aina mbalimbali ya figisu, ingawa hakuzianika lakini watapambana na kamwe Simba haitashuka kileleni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, leo, Hans Poppe amesema haitakuwa kazi rahisi kuishusha Simba kileleni.
“Kama ambavyo unaona, ligi imeisha mzunguko wa kwanza tukiwa kileleni. Nikuambie tutabaki hapo hadi mwisho,” alisema.

Hans Poppe alisema wanajua ugumu wa ligi hiyo, lakini Simba ina kikosi bora cha kuendelea kupambana hadi mwisho.

Simba ina pointi 35 kileleni, ikifuatiwa na Yanga yenye 33 ambayo ilicharuka mwishoni mwa ligi, Simba ikipoteza mechi mbili za mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV