November 30, 2016Kipa Kagera Sugar aliyesimamishwa na uongozi wa timu hiyo kupisha uchunguzi wa madai ya kuuza mechi, Hussein Shariff ‘Casillas’, amefunguka kuwa mpaka sasa yupo nyumbani na hakuna kiongozi yeyote yule ambaye amemfuata kwa ajili ya kulizungumzia suala hilo.

Casillas ambaye amewahi kuidakia Simba kwa msimu mmoja, alisimamishwa na uongozi wa timu hiyo inayonolewa na Mecky Maxime akiwa sambamba na beki Erick Kyaruzi baada ya timu hiyo kufungwa mabao 6-2 na Yanga kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Kipa huyo ambaye amebakiza mkataba wa miezi sita na timu hiyo, amesema tangu aliposimamishwa amekuwa nyumbani bila ya kufahamishwa chochote na viongozi hao juu ya hatima yake ya kurejea katika kikosi hicho.

“Mpaka sasa nipo nyumbani na sijui chochote kinachoendelea juu yangu kuhusiana na kurejea katika timu kwa sababu sijaambiwa wala sijataarifiwa lolote na viongozi tangu ambapo waliponisimamisha katika mzunguko wa kwanza.

“Na mkataba wangu sasa umebakia miezi sita pekee ya kuendelea kukipiga katika kikosi hicho lakini hata hivyo sitaki kuliongelea kwa undani suala hilo, nawasubiria wao juu ya uamuzi ambao watakuja kuutoa,”alisema Casillas ambaye aliwahi kuwa kipa bora msimu wa 2014/15.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV