July 19, 2021

5 COMMENTS:

  1. Naomba niwe wa kwanza hapa kutoa Maoni kuhusu usajili hasa kuhusu simba na Maoni Kama Maoni ni mawazo ya mtu binafsi anavyofikiria kwa hivyo povu rukhusa. Kwa TFF iongeze idadi ya wachezaji wa kigeni ili kuzipa timu zenye kushiriki kimataifa wigo Mpana zaidi wa kuwa na wachezaji wenye uwezo zaidi kimataifa isipokuwa kuwe na idadi maalum ya wachezaji wa kigeni kutumika kwa wakati mmoja uwanjani kwenye ligi ya ndani.
    (2) Simba ni kubwa na ina uwezo wa kufanya makunbwa Africa kuliko tunavyoichukulia watanzania wengi kuwa ni timu ya kawaida Sana. Ukitaka kujua uwezo na ukubwa wa soka wa Simba kwa sasa nenda kwenye marejeo ya mechi ya fainali ya CAF Kati ya kaizar chiefs na Ahly halafu achana na kiwango Cha chini alichoonesha kaizar Chiefs na kufanya moja ya fainali ya klabu bingwa Africa ya hovyo kabisa kuwahi kutokea kwenye miaka hii ya karibuni. Kilichonivutia zaidi mimi ni jinsi Simba ilivokuwa ikitajwa Mara kwa Mara na washereheshaji waliokuwa wakitangaza mechi ile Kama kwamba Simba ndio ilivokuwa ikicheza siku ile.
    (3) Ushauri kwa Simba ili kubakia na kiwango Chao bora na kuimarika zaidi.
    (a)Tulishauri Simba kumsajili straika mwenye nguvu na uwezo zaidi ya akina Boko na wenzake Kama simba walikuwa na nia ya dhati kutusua Africa kwenye nafasi za ziada za CAF lakini naona labda viongozi wa simba hawakuwa serious ipasavyo juu ya suala hilo. Sasa kufanya kosa ni kujifunza kosa ni kurejea kosa.Simba wasijizadharau hata kidogo wanaouwezo kabisa wa kubeba kombe la Africa wakati wowote kuanzia Sasa wakijipanga vyema, wakati umeshafika tayari.
    (2) Angalizo,C Mugalu na Rally Bwaliya ni moja ya matairi bora kuwahi kuingia Kwenye gari la Simba kinachohitajika ni jinsi ya kuyajaza upepo matairi haya sawa sawa ili kuja kulisukuma gari la Simba msimu ujao hasa kimataifa kwa Kasi zaidi. (Mapungufu ya Bwaliya) ni fitness tu peke yake katika physical structure. Simba wanatakiwa kufanya jitihada za makusudi kumsaidia Bwaliya kujenga mwili ulioshiba zaidi kwani ni moja ya dhahabu iliyokuwa bado kwenye vumbi.
    (Mugalu mapungufu yake) ni madongo Sana ili Simba kufaidika na uwezo halisi wa huyu mwamba. Mugalu ni hatari zaidi ya Bwaliya wa Ahly ya Misri hakuna ubishi juu ya hili. Ni bahati iliyowaangukia Simba kuwa na fowadi aina ya Mugalu kwani ana karibu kila kitu kuwa fowadi aliekamilika. Yupo vizuri hewani na aridhini ana nguvu ana Kasi na ball control ya kutosha tatizo bado hajawa na utulivu wa kutosha kwenye umaliziaji. Nini kifanyike ili awe bora? (1) Hajapata bado partnaship ya kaliba yake kuendena na staili yake ya uchezaji.(2) Anahitaji pia kuongezwa kujiamini zaidi japo kwa kudanganjwa kuwa yeye ndie straika namba moja ndani ya simba na timu mnatizama yeye kwa matokeo. Hii hali ya yeye kucheza huku akifikiria kukosea mwengine ataingia Mara nyingi inamuondeshea mchezaji kujiamini. Na ndio maana Kuna wakati Gomezi aliziba masikio yake kumpa Mugalu muda mwingi zaidi aliona kitu kwa Mugalu,Da Rosa anajua.
    Mwisho kwa Simba ni pongezi ila wajipange zaidi. Na Wachezaji wazawa hakuna njia ya mkato wanatakiwa kujiongeza zaidi kuendana na Kasi za akina chama la sivyo wataishia majungu.

    ReplyDelete
  2. Mdau umeongea vizuri sana ila kuna maeneo muhimu umeyasahau, nami ngoja nijazie nyama.Tatizo lingine la Simba ni kwenye kipa, hapa tunahitaji kipa wa kiwango cha kimataifa kwani Manula anafungwa magoli mepesi mno, hata wachezaji wetu wastaafu Mohamedi Mwameja na Zamoyoni Mogella , Golden boy waliwahi kusema kwamba ili Simba itusue kimataifa inahitaji kipa mwenye viwango kwani Manula anafungwa magoli mepesi.Sehemu ya pili ni upande wa Tshabalala, tunahitaji beki mwenye nguvu, kasi na anayeweza kupanda na kushuka kwa haraka sana.Tatizo la Tshabalala akipanda anachukua muda kurudi haraka, mfano match ya Simba na As Vita ugenini tuliona jinsi alivyoshindwa mpaka Luis akawa anamsaidia kukaba.Vile vile kosa alilofanya Simba kwa Kaizer Chiefs next season lisijirudie kwani tulicheza ugenini kwa kushambulia ambalo lilikuwa ni kosa kubwa mno, tungecheza kama tulivyocheza match za group stages, Kaizer Chiefs tungewatoa, kwani kwa Mkapa wasingetoka kabisa.Mwisho Coach Didier ashauriwe kuchukua maamuzi upesi, kwani amekuwa mgumu kuchukua maamuzi upesi, mfano match ya South Africa ilibidi baada ya kufungwa kipindi cha kwanza acheze defensive plan, match ya Yanga tulifungwa kwa uzembe wetu, dakika kmi za kwanza Nyoni mpira ulimkataa, ilikuwa amuingize Bwalya Magician, ndiyo maana alipoingia kipindi cha pili alibadirisha team ikawa inapanda.Mwisho, God bless Africa, God bless Simba.

    ReplyDelete
  3. Simba kimeo na wachumba tu hao. Mwaka kesho CAF CL mnaishia raundi ya kwanza. Ndiyo mtajua mugalu, bwalya wote vimeo

    ReplyDelete
  4. Hivi ninyi Wapenzi wa Simba hayo mambo yenu ya Usajili so mpeleke kwa Try and Try au mkawe Makocha humu hizo riwaya mnabore ,Tunga vitabu kwa ajili ya huo Usajili wenu.

    ReplyDelete
  5. Manula anatosha. Zimbwe ajiongeze. Nyoni ni mchezaji wa kitanzania huwaga hatuushikilii ubora wetu kwa kiwango kile kile kinachotakiwa, huo ndio ukweli.Ame ni kiungo mkabaji mzuri tu. Luhende anaweza kabisa kuwapa Simba wanachohitaji. Zimbwe Anahitaji mtu wa kumletea upinzani wa kweli. Dilunga sio winger midfielder ni kiungo mshambuliaji wa kati na huwa anacheza vizuri zaidi kwenye nafasi hiyo. Makocha wasaidizi akina Matola wawe wabunifu wa mawazo katika kuwashauri makocha wao wakuu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic