November 16, 2016

MKUDE


Baada ya hivi karibuni kuwepo kwa taarifa za wachezaji wawili wa Simba, kiungo, Jonas Mkude na beki wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kuhusishwa kutakiwa na Yanga, uongozi wa timu hiyo umekubali kuwaachia wakajiunge na klabu hiyo.

Muda mrefu sasa Yanga imekuwa ikihusishwa kuziwania saini za wachezaji hao kwa lengo la kutaka kikiongezea nguvu kikosi chao ambacho kwa sasa kinapambana vikali na Simba kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

KAHEMELE
Lakini pia inadaiwa kumtaka Mkude ili iweze kuimarisha safu yake ya kiungo hususan ile ya kiungo mkabaji ambayo imekuwa ikitesa kwa muda mrefu, kwa upande wa Tshabalala inamtaka ili akasaidiane na beki wake wa sasa wa kushoto, Haji Mwinyi.

Katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele amesema kama Yanga inawahitaji wachezaji hao basi inatakiwa kufuata taratibu za usajili na endapo watakubaliana basi wao wapo tayari kuwaruhusu kujiunga na timu hiyo.

Alisema Simba ni timu ambayo inajiendesha kisasa zaidi kwa kuzingatia taratibu za soka na hivyo kama kuna timu yoyote inahitaji mchezaji kutoka klabuni hapo, basi ifuate taratibu na endapo watafikia makubaliano watamruhusu mchezaji huyo kuondoka zake.

“Mkude na Tshabalala bado ni wachezaji wetu na  tuna mkataba nao na tunawapenda sana lakini kama  kuna timu yoyote inawahitaji na ikaleta dau lao mezani kwetu na likatuvutia tutawaruhusu waondoke.


“Kama Yanga wanawahitaji kweli waje tu tuzungumze tukikubaliana sisi hatuna tatizo tutawauzia kwa sababu wachezaji wote duniani wanauzwa, wakitupatia bilioni tatu au nne hiyo itakuwa safi kwetu kwani zitatusaidia katika mambo mengine ya maendeleo klabuni kwetu,” alisema Kahemele.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic