November 16, 2016Winga mwenye kasi wa Yanga, Simon Msuva ameweka bayana kwamba licha ya wapinzani wao Simba kuongoza kwenye Ligi Kuu Bara mpaka kumalizika kwa mzunguko wa kwanza lakini jambo hilo kwao haliwapi hofu yoyote kwani wanaamini watatumia mzunguko wa pili kufuta makosa yao yote na kutetea ubingwa wao.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa kombe la ligi katika mzunguko huu wa kwanza imemaliza nafasi ya pili ikiwa na pointi 33, mbili nyuma ya vinara Simba wanaofundishwa na Joseph Omog waliomaliza na pointi 35.

Kiungo huyo ambaye ameifungia Yanga mabao saba katika mzunguko huu amesema hawataki kuona wanapoteza ubingwa wa ligi kirahisi.

“Tunashukuru kumaliza mzunguko wa kwanza vizuri licha ya kwamba hayakuwa malengo yetu kumaliza nafasi ya pili lakini hata hivyo wapinzani wetu Simba ni kama tumewatanguliza na muda wowote ule tutarejea katika nafasi yetu.

“Yaani kwenye mzunguko huu unaokuja tunaingia na sera ya kwamba ni lazima wapinzani wetu watake wasitake waache pointi tatu kwa sababu tunataka kutoacha na kutopoteza pointi yoyote ile,” alisema Msuva.

SOURCE: CHAMPIONI0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV