November 14, 2016


Huku vikosi vingine vikianza mapumziko mafupi kabla ya ligi kuanza mzunguko wa pili, hali ni tofauti kwa timu ya Majimaji ya Songea ambayo imeweka wazi kuwa haitakuwa na mapumziko kwa wachezaji wake na badala yake wataendelea kujinoa kwa nguvu katika kipindi hiki.

Majimaji ambayo haikuwa na mwanzo mzuri wa ligi baada ya kupokea vipigo sita mfululizo katika mechi zao za awali za ligi, kwa sasa inakamata nafasi ya 13 kwenye ligi ikiwa na pointi 16 na imetoka katika hatari ya kushuka daraja baada ya timu hiyo kurudishwa kwa kocha Kally Ongala.

Ongala amesema ameamua kuchukua maamuzi hayo kutokana na kikosi hicho kutokuwa na maandalizi mazuri mwanzoni mwa msimu, jambo ambalo lilisababisha ipoteze mechi sita mfululuzo. Kabla ya Ongala, kocha wa timu hiyo alikuwa Peter Mhina aliyeiongoza katika mechi walizoboronga kwenye mzunguko wa kwanza.

“Tatizo kubwa la timu hii kufanya vibaya ilikuwa ni wachezaji kutokuwa fiti kabisa kwa sababu waliingia kucheza mechi bila ya kuwa na maandalizi mazuri mwanzoni, hivyo ikajikuta inacheza hovyo.

“Sasa kulifanya tatizo hilo kutojirudia, nimeamua katika kipindi hiki wengine wakipumzika sisi tufanye mazoezi ya kuhakikisha tunakuwa na uwezo zaidi ya hapa na hata ligi itakaporejea basi tunaondoka tulipo na kuifanya timu kuepuka kushuka daraja,” alisema Ongala.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic