November 14, 2016





Leo ni siku ya hukumu maana Azam FC itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting ambao ni maalum kwa ajili ya kupima uwezo wa nyota wao wa kimataifa walioletwa kwa ajili ya majaribio kabla ya kusajiliwa.

Azam imepokea jumla ya wachezaji saba kutoka Cameroon, Ghana na Ivory Coast ambao walianza kujaribiwa kwenye mchezo wa juzi Jumamosi dhidi ya JKT Ruvu na Azam kupoteza kwa mabao 2-0 lakini mchezo wa leo ndiyo utaamua nani anafaa kupewa mkataba.

Ofisa Mtendaji wa Azam, Saad Kawemba amesema baada ya mchezo huo, kocha Zeben Hernandez atawasilisha ripoti ya jumla kabla ya kuvunja kambi mpaka Desemba 3, mwaka huu ambapo wataanza maandalizi ya raundi ya pili.

Nyota hao ni mabeki: Mbimbe Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast) na kiungo Mpondo Stephane wa Cameroon. Washambuliaji ni Yaya Awaba Joel (Cameroon), Konan Oussou (Ivory Coast) na Waghana Samuel Afull na Benard Offori. 

“Nani abaki na nani aondoke, yote tumemuachia kocha, baada ya mchezo wa kesho (leo) atatupa ripoti yake ya jumla na tumedhamiria kuboresha kikosi chetu, kuna nyufa tumezibaini ndiyo maana tumeamua kufanyia kazi safu zote,” alisema Kawemba.

Aidha, Kawemba aliongeza kuwa tayari wamemalizana na wachezaji watatu wazawa ambao wataungana na kikosi Desemba 3, lakini hakuwa tayari kuwataja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic