November 9, 2016





Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja ameibuka na kusema kuwa ushindi wa mechi ya leo dhidi ya Tanzania Prisons ni muhimu kwa upande wao na unaweza kuonyesha dira yao kwenye ubingwa msimu huu.

Manyanja amesema kama timu yake itapata ushindi leo basi gepu la pointi kati yao na Yanga litakuwa linaridhisha na kuwapa mwanga wa ubingwa.

Simba inaongoza msimamo wa ligi kwa kuwa na pointi 35 nyuma ya Yanga yenye pointi 30, wakiwa wamepishana pointi tano, hivyo wanahitaji kuhakikisha wanapata pointi tatu leo.

Simba inashuka dimbani leo katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kuvaana na Prisons katika mchezo ambao unaaminika kuwa na ushindani mkubwa kufuatia timu zote mbili kuchapwa katika michezo yao iliyopita.

Mayanja alifunguka kuwa wamejiandaa ipasavyo kuhakikisha wanafanikiwa kupata ushindi mnono katika mchezo huo ambao utawasaidia katika kuhakikisha wanazipata pointi tatu.

”Mchezo wetu wa leo ni muhimu sana, tunahitaji kushinda ili kupata pointi tatu zitakazotusaidia kuendelea kuongoza kuwa na pointi tano wakati mzunguko wa kwanza ukiwa umemalizika.

“Iwapo tutapoteza basi tutakuwa na gepu dogo la pointi na wapinzani wetu jambo ambalo si sahihi kutokana na ushindani uliopo na iwapo wenzetu watashinda mchezo wao wa kesho ‘leo’.


“Kikosi kwa ujumla kipo vizuri kuna morali ya hali ya juu kwa wachezaji kuhitaji kushinda,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic