November 2, 2016Timu za Simba na Yanga, leo zinashuka uwanjani kutafuta pointi tatu katika viwanja tofauti ili kuhakikisha zinajitengenezea mazingira mazuri ya kuendelea kuwa juu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Simba ambayo ipo kileleni na pointi 32 ipo Shinyanga kucheza na Stand United wakati Yanga ambayo ipo nafasi ya pili na pointi 27 ipo jijini Mbeya kupambana na Mbeya City katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine.

Hata hivyo, wakati timu hizo zikiendelea na maandalizi ya mechi hizo, benchi la ufundi la Simba limeweka wazi kuwa linamuheshimu mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe kutokana na kazi yake kubwa anayoifanya uwanjani kwa sasa.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, alisema yeye kama mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Simba wanajua kuwa Tambwe ni mshambuliaji hatari hapa nchini kwa sasa na wamekuwa wakivutiwa na kazi yake anayoifanya.

“Ukweli sisi kama benchi la ufundi la Simba tunamheshimu sana Tambwe ni kati ya wachezaji mahiri kwenye Ligi Kuu Tanzania.

“Tazama tangu nimeanza kumfahamu sijawahi kumuona akiwa ameshuka kiwango kila siku yupo vilevile, hivyo ni kati wachezaji ambao washambuliaji wengine wanatakiwa kuiga mazuri yao,” alisema Manyaja.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV