Simba imefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Boko Veterani kabla ya kuwavaa African Lyon katika mechi ya 14 ya msimu wa Ligi Kuu Bara 2016-17.
Tayari Simba imecheza mechi 13 na kati ya hizo imeshinda 11 na sare mbili ikiendelea kubaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo.
Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 35 kileleni huku wakiwa wamepania kushinda mechi mbili zilizobaki.
Wachezaji wa Simba walionekana wakiwa na furaha na makini na mazozi hayo kabla ya kuivaa Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment