November 3, 2016

MBAO FC

Kagera Sugar imeamka, tena ugenini baada ya kuichapa Mbao FC kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mecky Maxime ambayo imeonekana kuboronga kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Kaitaba, ilionyesha soka la kuvutia na kuivurumisha Mbao FC ikiwa nyumbani Kirumba.

Mbao FC walionekana kucheza utafikiri wako ugenini huku Kagera Sugar wakimiliki zaidi mpira na kutawala hasa sehemu ya kiungo.

Kagera Sugar wangeweza kupata mabao zaidi kama wangekuwa makini.

Upande wa Mbao FC, uongozi wa benchi lao la ufundi ulilalamika kwamba walikuwa na uchovu wa kusafiri mfululizo kutokana na ratiba yao kuwa inayowaminya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV