November 3, 2016


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerry Tegete ameibuka tena baada ya kupachika mabao mawili wakati Mwadui FC ikivaa Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, leo.

Tegete ambaye aliingia kipindi cha pili na kufunga mabao hayo, hakuweza kuisaidia Mwadui FC ambayo sasa 'watu wamekuwa wanajiokotea tu'.

Wakati anafunga bao la kwanza, tayari Mtibwa Sugar walikuwa na mabao matatu ya Haruna Chanongo na Rashid Mandawa.

Tegete ameadimika kutokana na kuandamwa na majeruhi lakini alikuwa mmoja wa washambuliaji waliokuwa wanategemewa kuwa lulu ya taifa hasa katika ufungaji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV