November 3, 2016
Pamoja na kupata ushindi kutoka kwa timu ngumu ya Stand United, Simba wameendelea kusisitiza kamwe hawataidharau African Lyon.

Simba inashuka dimbani Jumamosi kuivaa Africa Lyon ikiwa ni siku chache baada ya kuitwanga Stand United kwa bao 1-0 na kufikisha ushindi wa 11 katika msimu huu.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema wanaamini Lyon ni kati ya timu ngumu za Ligi Kuu Bara.

"Tunajua Lyon ni timu ngumu sana, lakini tunachotaka sisi ni kushinda na kupata pointi tatu.

"Hakuwezi kuwa na ushindi rahisi. Hakuna timu laini, hivyo tutaendelea kucheza kila mechi kwa kujituma na malengo ili tushinde," alisema Mgosi.

Simba ilitarajiwa kurejea Dar es Salaam leo ikitokea Shinyanga kupitia Mwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV