Straika Amissi Tambwe na nahodha wa Yanga, Haruna Niyonzima, kwa pamoja wamesema kufungwa na Mbeya City hakujawakatisha tamaa ya kutetea ubingwa wao na kamwe Simba wasijidanganye.
Yanga ilichapwa mabao 2-1 katika mechi yao ya mwisho kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa.
“Simba wasijidanganye kuhusu ubingwa eti kwa sababu wanaongoza, bado kuna mechi nyingi mno ambazo zinaweza kuwaweka chini na sisi tukaibuka,” alisema Tambwe.
Lakini Niyonzima raia wa Rwanda akasisitiza, wamepoteza mechi mbili ambalo si jambo zuri lakini ni mapema sana kuanza kumtaja bingwa.
“Kupoteza mechi mbili inauma sana, lakini hiyo si sababu ya kupoteza ubingwa na Simba japokuwa wanaongoza ligi wasidhani sisi tumelala, hapana kilichotokea kwetu ni bahati mbaya tu.”
Non sense, kwahiyo mnafikiria simba watalala nyie mkiamka. Mwaka huu hakuna viporo mlivyozoea.
ReplyDeleteNon sense, kwahiyo mnafikiria simba watalala nyie mkiamka. Mwaka huu hakuna viporo mlivyozoea.
ReplyDeletemazoea mabaya kweli kweli,kwa uchezaji wenu yeboyebo mtagongwa tu sana
ReplyDelete