November 5, 2016

MINGANGE

Kocha wa Prisons, Meja Mstaafu Abdul Mingange amewaonya wachezaji wake kutoidharau Yanga kwa kuwa ilifungwa na Mbeya City.

Meja huyo mstaafu amesema Yanga kupoteza dhidi ya Mbeya City ni ugumu kwao kwa kuwa haitataka kupoteza mara mbili mjini Mbeya.

Yanga itakuwa mgeni wa Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, kesho. Ikiwa ni siku chache baada ya kufungwa na Mbeya City kwa mabao 2-1.

“Watu wasione Yanga sababu imefungwa na Mbeya City basi na sisi ni lazima tuifunge, soka halipo hivyo lakini hatutakubali kufungwa na Yanga.

“Yanga ni timu kubwa yenye uzoefu na inayojua kupambana, sasa mashabiki wategemee soka la ushindi uwanjani ila wasidhani kama kila kitu ni kirahisi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV