November 7, 2016

BUKUNGU (ALIYESUKA), AKIWA NA WACHEZAJI WENGINE WA SIMBA.

Kocha Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amewataka viongozi wa timu hiyo kuhakikisha beki wake wa kulia, Mcongo, Javier Bokungu anaongezewa mkataba ili aendelee kuitumikia timu hiyo katika harakati zake za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.
Bokungu ambaye alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu, alikuwa na mkataba wa miezi sita tu wa kuitumikia timu hiyo ambao alipewa baada ya baadhi ya viongozi pamoja na Omog mwenyewe kutokuwa na imani naye juu ya kiwango chake.
Hata hivyo, Omog amesema kuwa mawazo yao hayo waliyokuwa nayo juu ya Bokungu yalikuwa tofauti kwani wangefanya makosa makubwa sana kama wasingemsajili.
Alisema uwezo mkubwa anaouonyesha uwanjani, hakuna beki yeyote wa kulia katika michuano ya ligi kuu mpaka sasa ambaye ni bora zaidi yake.

“Kiwango chake kwa sasa kipo juu na anafanya vizuri kila siku, hakika ningefanya makosa kama nisingemsajili.

“Anacheza kwa kutumia akili, pia na uzoefu mkubwa na anajua kukabiliana na kila mchezaji anayekutana naye, kama ana makosa ni kidogo sana ambayo najitahidi kumweka sawa ila napenda kuendelea naye katika kikosi changu, kama mkataba wake upo mbioni kumalizika basi niwaombe tu viongozi wamuongezee,” alisema Omog.

SOURCE: CHAMPIONI JUMATATU


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV