November 19, 2016Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino ana mpango wa kuiimarisha michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa klabu, ifikie kuwa na timu hadi 32.

Infantino anataka timu ziongezeke kutoka saba hadj 32 ili kuongeza utamu na mpango wake anataka uanze mwaka 2019.

Infantino ameliambia gazeti la michezo la Gazzetta dello Sport na lile la El Mundo Deportivo kwamba anaamini hilo linawezekana.


Michuano ya Kombe la Dunia la klabu mwaka 2015 iliyofanyika nchini Japan kama ilivyo ada, iliingiza faida kupitia matangazo kiasi cha dola million 20 ambacho kilionekana ni kiasi kidogo kwa kuwa michuano ya mwaka 2014 iliyofanyika nchini Morocco iliingiza hadj cola million 40.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV