November 19, 2016
Uongozi wa Simba umesema kuwa baada ya kumalizana na beki wake wa kushoto, Mohammed Hussein Zimbwe maarufu kama‘Tshabalala’ kuhusiana na kuongeza mkataba mpya, pia umedai kumalizana na kiungo wake, Jonas Mkude ambaye pia mkataba wake unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa kuwa Mkude pamoja na Tshabalala walikuwa na mpango wa kutaka kujiunga na Yanga kutokana na mikataba yao kufika tamati.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alisema kuwa Mkude tayari wameshamalizana naye kama ilivyo kwa Tshabalala, hivyo ataendelea kuitumikia klabu hiyo.


“Mkude pia tumeshamalizana naye kama ilivyo kwa Tshabalala, hivyo ataendelea kuwa kikosini kwa sababu mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo taarifa zote kuhusiana na mchezaji huyo hazina ukweli wowote,” alisema Hans Poppe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV