November 8, 2016

SIMBA WAKIWA KWENYE UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM KWA SAFARI YA MBEYA

Kikosi cha Simba kimetua salama salimini mjini Mbeya tayari kwa ajili ya mechi yao ya kesho dhidi ya Prisons.


Simba inayoongoza Ligi Kuu Bara, imetua Mbeya ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya African Lyon.

Kipigo hicho ni cha kwanza kwa Simba ambayo ilikuwa imecheza mechi 13 bila ya kupoteza hata moja. Ikiwa imeshinda 11 na sare mbili.


Kwa upande wa Prisons nayo, ina kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 pia kutoka kwa mabingwa watetezi Yanga, maana yake itakuwa mechi ngumu hasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV