November 8, 2016


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu amelazimika kubaki jijini Dar es Salaam wakati Simba ikisafiri kwenda Mbeya kuivaa Prisons kutokana na msiba alioupata.

Ajibu amepata msiba wa mwanaye baada ya mpenzi wake kujifungua na bahati mbaya mtoto kufariki dunia.

Kutokana na msiba huo, uongozi wa benchi la ufundi uliamua kumpumzisha Ajibu ambaye hata hivyo hivi karibuni amekuwa hana uhakika katika kikosi cha kwanza cha Simba.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amethibitisha kuhusiana na msiba alioupata Ajibu.

"Kweli Ajibu amepata msiba wa mwanaye, hivyo yeye amebaki Dar es Salaam na sisi tumesafiri hadi Mbeya kuendelea kupambana kwa niaba yake na Wanasimba wote," alisema Mgosi.


Simba ipo mjini Mbeya kuivaa Prisons katika mechi itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Sokoine na ndiyo itakuwa ya kufunga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara.

1 COMMENTS:

  1. Me sijaelewa hapa Saleh,hv Kwenye kifo kuna bahati Mbaya?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV