November 30, 2016


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, amefanikiwa kumaliza mgogoro uliozua hofu ya kutokuwepo kwa pambano la Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ na Francis Cheka lililopangwa kufanyika Desemba 25, mwaka huu kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar.

Kutokana na kuwepo kwa mgogoro huo, iliwalazimu viongozi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), kutinga kwenye ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kumaliza mgogoro huo kama walivyotakiwa kufanya hivyo na Nape.

Kaike Siraju ambaye ni promota wa pambano hilo, 
amesema: “Tunamshukuru Waziri Nape kwa kusimamia mgogoro huu na kuumaliza kabisa, sasa pambano lipo palepale kama lilivyopangwa, hivyo tunawashukuru wote walioshiriki katika kupigania kumaliza tofauti zilizojitokeza.


“Mashabiki wa masumbwi popote walipo wasiwe na wasiwasi, Desemba 25 waje pale PTA kushuhudia pambano hilo kali na tayari nimepata taarifa kwamba mabondia wote wanajifua vikali kila mmoja akitaka kumshinda mwenzake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic