December 2, 2016
Kiungo mshambuliaji wa wa Yanga, Malimi Busungu, juzi Jumatano alijikuta katika wakati mgumu katika mazoezi ya timu hiyo baada ya kuwekwa mtu kati na uongozi wote wa benchi la ufundi la timu hiyo.

Busungu alitoweka klabuni hapo baada ya mechi yao dhidi ya Simba, Oktoba Mosi, mwaka huu, awali ilielezwa kuwa alitoweka kutokana na kukasirishwa na kutopata nafasi kikosini hapo lakini ikadaiwa kocha wake msaidizi, Juma Mwambusi anamhujumu.

Mara baada ya mazoezi ya juzi, Busungu aliitwa na Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina aliyekuwa na Mwambusi, Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi, Hans van Der Pluijm, Kocha wa Makipa, Juma Pondamali na meneja wa timu, Hafidh Saleh wakazungumza kwa dakika 15 na mchezaji huyo.

Katika kikao hicho, Lwandamina hakuwa muongeaji mkubwa zaidi ya Mwambusi ambaye ndiye alionekana kuwa bize kuongea akisaidiwa na Pluijm huku meneja wa timu na kocha wa makipa wakichangia kidogo.


Baada ya kumaliza, Championi Ijumaa lilimtafuta mchezaji huyo ambaye alifunguka hivi: “Kile kikao kilikuwa cha kawaida, nikiwa kama mchezaji wao ni lazima nizungumze nao kama vile, hakuna kibaya zaidi kilichotokea."

SOURCE: CHAMPIONI 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV