Hatimaye wachezaji wa Yanga wameanza rasmi mazoezi leo ikiwa ni baada ya kugoma kwa siku mbili.
Wachezaji hao waligoma kwa siku mbili wakidai kulipwa mshahara wao wa mwezi uliopita. Hawakufanya mazoezi juzi na jana.
Lakini hivi punde, wachezaji hao wameanza mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam chini ya Kocha George Lwandamina.
Wamerejea mazoezini baada ya kufikia mwafaka na kuelewana na uongozi kuwa utahakikisha unawalipa kabla ya mechi yao ya keshokutwa Ijumaa dhidi ya African Lyon.







0 COMMENTS:
Post a Comment