Wachezaji wa Yanga wamesema wamemalizana na uongozi wao kuhusiana na tofauti zilizojitokeza na wataanza rasmi mazoezi leo.
“Kweli tumemalizana, unajua sisi ni binadamu. Mambo ya mgongano yanatokea, tunajua hata maofisini kwenu yanatokea.
“Sasa tumerekebisha na leo kwa pamoja tutarejea mazoezini tayari kuanza kazi,” alisema mmoja wa wachezaji wakongwe wa Yanga.
Mchezaji mwingine kutoka nje ya Tanzania, ameiambia SALEHJEMBE: “Nilikuwa najiandaa kwenda mazoezini, leo tutaanza jioni kwa kuwa hakuna tofauti tena na uongozi.”
Wachezaji wa Yanga waligoma kufanya mazoezi kwa siku mbili mfululizo, juzi na jana kwa madai ya kucheleweshewa mshahara wao wa mwezi uliopita.
Awali uongozi wa Yanga kupitia Katibu wake Mkuu, Baraka Deusdedit ulikuwa ukikanusha hata hivyo baadaye ulikubali kwamba mambo hayakuwa mazuri na suala hilo wanalishughulikia.







0 COMMENTS:
Post a Comment