December 3, 2016



Kikosi cha Medeama cha Ghana imepoteza wachezaji watatu ambapo wawili Enock Agyei na Daniel Amoah wamejiunga na Azam FC huku Kipa Daniel Agyei akiwa mbioni kujiunga na Simba.

Kiungo wa Medeama, Gordon Joseph amesema kati ya wachezaji hao watatu pigo kwao ni kuondoka kwa Agyei kwani alikuwa tegemeo kikosini.

Agyei aliwasili nchini Jumatano wiki hii tayari kupewa mkataba na siyo kufanya majaribio kama ambavyo wachezaji wengine waliojiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu ambao ni Besala Bokungu, Frederic Blagnon, Method Mwanjale na wengineo.

Joseph alisema awali kuondoka kwa Amoah mwanzoni mwa msimu kidogo hakukuwa na pengo kubwa lakini kuondoka kwa Agyei na Enock aliyetua rasmi Azam, ni pengo kubwa ndani ya kikosi chao.

“Wote walikuwa watu muhimu. Amoah alipoondoka benchi la ufundi liliangalia jinsi ya kuziba pengo lake lakini kwa Enock na Danny, ukweli wametumaliza,” alisema na kutoboa siri kumbe jamaa alikuwa akiwaniwa pia na timu nyingine za Ghana, ikiwemo Wa All Stars ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Ghana.

“Sawa, tumekuwa naye kwa muda mfupi, alikuwa Afrika Kusini lakini ndiye alikuwa hatari sana kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (Caf).

“Binafsi nilijua atakwenda Wa All Stars maana pia walikuwa wanamhitaji lakini ndiyo hivyo, hiyo timu anayokuja kuchezea (Simba) itanufaika naye,” alisema kiungo huyo.


Agyei pia alitakiwa na Free States ya Afrika Kusini na Bechem United ya nchini kwao Ghana, lakini akazichomolea zote na kutua Simba.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic