Mshambuliaji Fredric Blagnon amesalimika na atabaki kuendelea kuichezea Simba.
Blagnon alikuwa kwenye kundi la wachezaji wanaotemwa Simba na uongozi wa klabu hiyo uliamua kufanya hivyo kwa kuwa alishindwa kuonyesha cheche.
Kutokana na hali hiyo, uliamua kumbakiza Ame Ali ambaye alikuwa akilalama kutopata nafasi ya kucheza ili aipate na kuisaidia Simba.
Lakini baada ya kwenda mapumziko, Ame amekataa kurejea Simba kwa madai hapati nafasi ya kutosha ya kucheza.
Simba mwisho wameamua kumbakiza Blagnon kwa kuwa kama watamuacha wakati Ame amegoma kurejea, maana yake hawatakuwa na mshambuliaji mzoefu.
“Kweli mwisho tumeamua abaki, maana Ame amekataa kurejea,” kilieleza chanzo.
Kuthibitisha hilo, tayari Blagnon yuko na kikosi cha Simba mjini Mtwara akisubiri kuivaa Ndanda, Jumapili.








0 COMMENTS:
Post a Comment