Klabu ya Mbeya City na mshambuliaji Mrisho Ngassa wamekubaliana katika suala la usajili lakini bado hajamwaga wigo.
Lakini hofu ili kuwahi dirisha linalofungwa hivi punde, wamekubaliana Ngassa jina lake lijumuishwe kwenye usajili utakaotumwa TFF.
Mbeya City na Ngassa wamekubaliana katika suala la usajili kwanza, kwamba jina lake litumwe halafu baada ya hapo, kesho ndiyo asaini.
“Wahusika katika masuala ya usajili walikuwa bize na majukumu mengine, hivyo hawakupata muda wa kutosha kuzungumza na Ngassa ambaye tayari yuko Mbeya,” kilieleza chanzo, rafiki wa Ngassa.
Tayari Ngassa yuko Mbeya kwa ajili ya masuala hayo ya usajili na kabla, alikuwa ndiyo amejiunga na Fanja ya Oman, hata hivyo bado haijajulikana kuhusiana na mkataba wake.
Taarifa nyingine zimeeleza, Mbeya City wameamua kufanya hivyo, kutuma jina lake kabla ya kumsajili ili kupata uhakika kwanza kuhusiana na usajili wake kwa kuwa walikuwa wakiwasiliana na Fanja ili kupata uhakika.








0 COMMENTS:
Post a Comment