Baada kuzagaa tetesi za winga wa Yanga Simon Happygod Msuva kuhusishwa kutua Simba , mabosi wa Yanga, wameamua kumpiga ‘stop’ nyota huyo kuongelea lolote juu ya maisha yake ya soka likiwemo suala zima la usajili.
Msuva ambaye hivi karibuni alikaririwa na Championi Jumatano, akianika dau lake endapo Simba watamhitaji, amepigwa pini kuongea na vyombo vya habari hasa juu ya masuala yoyote yahusuyo usajili wake, huku akiambiwa akiendelea kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali.
“Dah! ama kweli Yanga kwa sasa wameamua kufanya mambo yao ‘siriaz’ maana si kwa mwendo huu hadi sasa inafikia hatua hata wachezaji wao wanaanza kuishi kwa uoga, huwezi kuamini tangu Msuva aonekane anaongea na vyombo vya habari sasa ametaitiwa kiasi kwamba haruhusiwi tena.
“Juzi kati kuna baadhi ya mabosi wa Yanga, walimpigia simu na wengine kumfuata, wakimtaka aachane na mambo ya kuongea na ‘media’ hasa mambo ya usajili, jambo hilo limevaliwa njuga utadhani kaharibu sijui nini vile, huwezi kuamini hadi bosi wa timu naye amemchimba mkwara huo,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kupenyezewa ishu hiyo, tuliamua kumtafuta Msuva mwenyewe kwa ajili ya kuweka mzani sawa, ambapo baada ya kumpata, alikiri wazi kukatazwa kuongea lolote huku akishindwa kudhibitisha ni kiongozi gani aliyemzuia.
“Yaah kweli uongozi wangu umeniambia nipumzike kuongea na vyombo vya habari, badala yake kama kuna mtu ana shida basi ni vyema akawasiliana na kiongozi yoyote wa juu wa klabu yangu, maana kwa sasa tupo bize na maandalizi ya mzunguko ujao,” alisema Msuva ambaye alikuwa mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara 2014/2015.
SOURCE: CHAMPIONI
Baada ya kupenyezewa ishu hiyo, tuliamua kumtafuta Msuva mwenyewe kwa ajili ya kuweka mzani sawa, ambapo baada ya kumpata, alikiri wazi kukatazwa kuongea lolote huku akishindwa kudhibitisha ni kiongozi gani aliyemzuia.
ReplyDeletehapa tayari keshangea tena