Mshambuliaji aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, Obrey Chirwa raia wa Zambia, anadaiwa kuendelea kufanyiwa mpango wa kurejeshwa kwa mkopo katika timu yake hiyo ya zamani ili nafasi yake iweze kuchukuliwa na Mzambia mwenzake, Winston Kalengo, anayekipiga katika timu ya Leopard ya Congo Brazaville.
Chanzo chetu makini kimeeleza kuwa, mabosi wa Yanga wanaendelea kufanya mchakato wa kumtoa Chirwa kwa mkopo, lengo ni kumpisha Kalengo, ambaye anatarajiwa kudondoka siku yoyote kuanzia leo ili kuiwezesha klabu hiyo kujiweka sawa zaidi kwenye upande wa upachikaji wa mabao.
“Kuna jambo kweli linaendelea ndani ya klabu ambapo viongozi wetu wakuu tangu jana walikuwa wanaendelea kufanya mipango ya kumuombea Chirwa ili aende kwa mkopo FC Platnaum na lengo lao kubwa ni kumshusha yule straika anayekipiga Congo.
“Ujue Yanga bado haijitoshelezi sana kwenye safu ya ushambuliaji na ndiyo maana utaona wanafanya juu chini ili waweze kuongeza watu wa nguvu kwenye nafasi hiyo, kwani uwezo wa Chirwa bado haujawavutia kiasi hicho, ,” kilisema chanzo hicho.
Chirwa ambaye alianza vibaya ndani ya Yanga kiasi kuonekana ni mzigo, katika mechi za mwisho mwisho za kumaliza mzunguko wa kwanza alionyesa kiwango kizuri na kufanikiwa kufunga mabao manne kwenye ligi mpaka sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment