ISMAIL WAKATI AKIWA NCHINI MAREKANI |
Kesho Jumamosi Desemba 10, 2016 kutakuwa na mchezo maalumu wa kirafiki utakaozikutanisha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara Mbao FC na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni utakuwa ni maalumu kwa ajili ya kutoa heshima kwa marehemu Ismail Khalfan - mchezaji wa timu ya vijana Mbao aliyefariki dunia Desemba 4, mwaka huu wakati akiiitumikia timu yake ya vijana kwenye mchezo wa Ligi ya Vijana ya TFF U20 dhidi ya Mwadui, uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Mbali ya kutoa heshima kwa marehemu Khalfan, pia waratibu wa mchezo huo wakiwamo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), wamepanga mapato yake yote ni kutoa rambirambi kwa familia ya Khalfan iliyopoteza ndugu yao mchezoni.
TFF, KRFA, MZFA na wadau wengine wangali wakitoa pole kwa familia kwa msiba kwa familia kwa msiba wa Ismail Khalfan ambaye pia ameombolezwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Rais wa CAF, Issa Hayatou.
Kadhalika, mchezo huo utatumika kama kuzipima nguvu timu hizo baada ya mapumziko ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) hivyo wadau wote wa michezo wameombwa kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuchagia rambirambi ya familia hiyo ambayo kwa pamoja na wanafamilia ya soka walipoteza hazina nyingine muhimu kwenye mpira wa miguu.
0 COMMENTS:
Post a Comment