PONDAMALI |
Klabu ya Simba imemsajili kipa Mghana, Daniel Agyei aliyetokea Medeama ya nchini kwao, hata hivyo Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali amempopoa kuwa ni kipa wa kawaida sana na hajaona sababu ya usajili wake.
Akieleza utetezi wa kauli yake, Pondamali mwenye weledi mkubwa golini, alisema kipa anayeruhusu mabao matano kwa timu moja kama alivyofungwa na TP Mazembe pia Yanga wakifunga mawili ni kipimo kizuri cha ubora wake.
Pondamali alikutana na Agyei kwenye Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi na timu zote kuishia hatua hiyo huku TP Mazembe na MO Bejaia zikipeta.
MAYANJA |
Anasema hajaona kishawishi chochote cha Simba kumchukua ilhali wanaye kipa mwingine wa kimataifa, Muivory Coast, Vincent Angban.
“Namjua vizuri, sisi tulimfunga mabao mawili (sare ya bao 1-1 jijini Dar na Yanga kupoteza kwa mabao 3-1 huko Ghana), lakini pia utamuitaje kipa bora mtu aliyefungwa mabao matano na timu moja?
“Mazembe walimfunga mabao matatu pale Lubumbashi, kule kwao Ghana akafungwa mabao mawili. Sioni kama ni kipa wa kutisha kiasi kwamba wawe na makipa wawili wa kimataifa ingawa sitaki kuingilia zaidi kwenye hilo.
AGYEI AKISAINI SIMBA |
“Kwangu hana tofauti na uwezo wa Dida ama Barthez wangu,” alisema kipa huyo wa zamani wa Taifa Stars.
Mayanja amjibu Pondamali
Aidha Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda Jackson Mayanja ‘Mia Mia’ amekuja juu na kufungukia usajili huo kuwa ni kutaka kuwa na makipa wenye uwezo sawa kwa ajili ya kupokezana.
Mia Mia aliongeza kuwa awali Angban alikuwa hana mbadala na kwamba kuna baadhi ya mechi ambazo alicheza tu ilmradi kwa sababu tu alichoka ama kutokuwa fiti.
“Haimaanishi kwamba Angban ndiyo anaachwa, tulitaka kuimarisha zaidi nafasi ya ukipa. Angban hakuwa na msaidizi na kiufundi raundi ya kwanza kuna sehemu ilionekana kabisa anatakiwa kupumzika lakini kwa kuwa hakukuwa na mbadala alicheza tu.
Uwepo wa Agyei ni changamoto kwenye nafasi hiyo, yeyote anaweza kuanza,” alisema kocha huyo wa zamani wa Kagera, Coastal na Kiyovu Sport ya Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment